1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Maafisa wa Gaza wasema watu 60 wameuawa kwenye mashambulizi

15 Januari 2024

Maafisa katika Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Hamas wamesema watu kadhaa wameuawa usiku wa kuamkia leo katika mashambulizi makali ya Israel.

https://p.dw.com/p/4bFCo
Mashambulizi ya karibuni yaliilenga miji ya kusini ya Khan Yunis na Rafah pamoja na maeneo yaliyo karibu na Mji wa Gaza.
Mashambulizi ya karibuni yaliilenga miji ya kusini ya Khan Yunis na Rafah pamoja na maeneo yaliyo karibu na Mji wa Gaza.Picha: Mahmoud Sabbah/AA/picture alliance

Hayo ni wakati vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ambavyo vimeitikisa kanda nzima vikifikisha siku 100.

Wizara ya Afya ya Gaza imeripoti vifo vya watu 60 iliowaita mashahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa kote katika ukanda huo.

Ofisi ya habari ya serikali ya Hamas imesema hospitali mbili, shule ya wasichana, na makaazi kadhaa yalishambuliwa usiku kucha.

Mashambulizi ya karibuni yaliilenga miji ya kusini ya Khan Yunis na Rafah pamoja na maeneo yaliyo karibu na Mji wa Gaza.

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake viliyalipua magaidi wawili waliokwua wakipakia silaha ndani ya gari katika mji wa Khan Yunis, na kukivamia kituo cha kamandi ya Hamas na kukamata silaha.

Machafuko makali katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel na kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, pamoja na mapigano kati ya vikosi vya Marekani na waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran.