Maafisa wa Ukraine wamemjibu Papa Francis
11 Machi 2024Matangazo
Maafisa wa Ukraine na washirika wao wamekosoa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis kwa kusema kwamba Kyiv inapaswa kuwa na "ujasiri" wa kujadili kumalizika kwa vita na Urusi, kauli ambayo wengi waliitafsiri kama wito kwa Ukraine kusalimu amri.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine na Poland, mshirika mkubwa wa Kyiv, walilaani matamshi ya Papa. Lakini pia jana, Jumapili hiyo, kiongozi wa moja ya makanisa ya Kikristo nchini Ukraine alisema lazima taifa lijihami na uvamizi wa Urusi ulioanza Februari 24, 2022.
Katika ibada maalumu ya Jana Jumapili PapaFrancis ambae mara zote ameonekana kuchukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine na Urusi alisema anaiombea aman Ukraine.