1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya serikali yatanda Israel

11 Julai 2023

Maandamano yamezuka kote nchini Israel masaa chache tu baada ya bunge kupitisha kifungu muhimu cha mpango wa mageuzi katika idara ya mahakama ambayo wapinzani wanasema ni hatua inayotishia demokrasia.

https://p.dw.com/p/4Tin9
Israel Tel Aviv | Protest gegen Justizreform
Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Waandamanaji walifunga barabara na kukusanyika katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv, huku watu 42 wakiripotiwa kukamatwa.

Polisi imesema katika taarifa kuwa, wanaruhusu uhuru wa kuandamana japo kwa watu kuzingatia sheria na kudumisha utulivu.

Soma zaidi: Wanajeshi wa Israel waondoka mjini Jenin

Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu iliendelea na mpango huo wa mageuzi katika idara ya mahakama licha ya maandamano makubwa kufanyika tangu mapendekezo ya mageuzi hayo yalipotangazwa mnamo mwezi Januari.