SiasaKosovo
Maandamano mapya ya WaSerbia yaibuka Kosovo
31 Mei 2023Matangazo
Hata hivyo, tovuti ya habari ya koha.net umeripoti kuwa hali imeendelea kuwa tulivu. Ghasia kati ya wanamgambo wa Serbia na ujumbe wa kulinda amani wa Jumuia ya Kujihami ya NATO, KFOR huko Zvecan yalisababisha majeraha kwa wanajeshi 30 na Warsebia 50. Awali, NATO ilitangaza kupeleka wanajeshi zaidi 700 ili kukisaidia kikosi cha wanajeshi 3,800 kilichoko Kosovo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken ametoa wito wa kuwepo utulivu. Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Marekani, CNN, Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti amesema anahitaji kuwa na askari polisi wanaotetea utawala wa sheria, wanaolinda utulivu, amani na usalama.