1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi yafanyika Ufaransa

9 Julai 2023

Zaidi ya watu 2,000 walikusanyika jana katikati mwa Paris nchini Ufaransa, kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha kijana Adama Traore kilichotokea mwaka 2016 licha ya marufuku ya mahakama.

https://p.dw.com/p/4TdHq
France protesters defy bans to rally against police violence
Picha: Thomas Padilla/AP/picture alliance

Maandamano  yalifanyika pia kwenye maeneo mengine kote nchini Ufaransa ili kupinga ukatili wa polisi na kuenea kwa ubaguzi wa rangi, huku hali ya wasiwasi ikizidi kuongezeka baada ya nchi hiyo kukumbwa na machafuko siku kadhaa zilizopita.

Ufaransa imekuwa ikikabiliana na ghasia zilizotokana na mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 17 mwenye asili ya Algeria yaliyofanywa na polisi kwenye kituo cha trafiki mnamo Juni 27.

Soma zaidi: Hamkani bado si shwari Ufaransa kufuatia kifo cha Nahel

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imekataa madai yaliyotolewa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi kwamba nchi hiyo inakabiliwa na ubaguzi wa rangi wa kimfumo na matumizi ya nguvu ya polisi.