1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya kuliunga mkono jeshi yafanyika Niger

20 Agosti 2023

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Niger Niamey, kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi uliyopita, ambayo kiongozi wake ameonya dhidi ya mataifa ya nje kuingilia masuala ya ndani ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4VNUf
Niger Niamey | Abdourahamane Tiani
Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP

Waandamanaji walitoa maneno ya kuishutumu Ufaransa, mtawala wa zamani wa Niger, pamoja na Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS inayotafakari kuiingilia kijeshi nchi hiyo ili kurejesha utawala wa rais Mohamed Bazoum iwapo majadiliano na viongozi walioipindua serikali yatafeli.

Papa Francis atoa wito wa upatikanaji amani Niger

Mabango yalikuwa na ujumbe wa "komesha uingiliwaji kijeshi na hapana kwa vikwazo" yakimaanisha vikwazo vya kifedha na kibiashara vilivyowekwa na ECOWAS siku nne baada ya mapinduzi.

Maandamano ya leo yalihudhuriwa pia na wasanii waliyousifia uongozi huo wa kijeshi.