1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano ya upinzani nchini Congo yatawanywa na polisi

Saleh Mwanamilongo
15 Septemba 2021

Wafuasi kadhaa wa chama cha upinzani cha Ecidé cha Martin Fayulu wamekamatwa na wengine kujeruhiwa kufuatia maandamano hayo ambayo yalitawanywa na polisi.

https://p.dw.com/p/40M5O
Kongo, Kinshasa: Wahlen im Kongo
Picha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Maandamano yalioitishwa na mfanyibiashara na mwanasiasa maarufu wa upinzani Martin Fayulu yametawanya na polisi mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maandamano hayo yalilenga kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi, na kwenye mahakama ya katiba. wafuasi kadhaa wa chama cha Fayulu wamekamatwa na wengine kujeruhiwa mjini KInshasa na kwenye miji mingine ya Congo.