Maandamano yaendelea Georgia kwa siku ya saba mfululizo
5 Desemba 2024Waandamanaji hao walifunga barabara kuu ya Rustaveli na kutoa wito wa muendelezo wa sera zinazouunga mkono Umoja wa Ulaya kwa taifa hilo, kufuatia uamuzi wa chama tawala kinachoiunga mkono Urusi, Georgian Dream ambao umekwamisha mchakato wa Georgia kuelekea kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Soma pia: Waandamanaji Georgia wakabiliana na polisi
Shirika la habari la Associated press limeripoti kuwa waandamanaji hao wanasema chama tawala kimeisaliti Georgia na kuirudisha nchi hiyo kwenye uhusiano wa karibu na Urusi.
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, msemaji wa mkuu mpya wa sera za nje za Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, ametaja ripoti za kutisha za kukamatwa kiholela, vurugu, na unyanyasaji wa waandamanaji na kuhimiza pande zote kutojihusisha na vurugu.