1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko ya tabia nchi yatishia ustawi wa watoto duniani

Sylvia Mwehozi
19 Februari 2020

Mustakabali wa kila mtoto ulimwenguni uko hatarini kutokana na mataifa kote ulimwenguni kushindwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.

https://p.dw.com/p/3XysA
Ghana Project BG Ghana's viele Gesichter
Picha: Imago/F. Stark

Mustakabali wa kila mtoto ulimwenguni uko hatarini kutokana na mataifa kote ulimwenguni kushindwa kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kutoa mazingira safi na yenye afya kwa ustawi wao,  kulingana na ripoti iliyotolewa na  na Umoja wa Mataifa.

Wakati watoto katika mataifa tajiri wana nafasi nzuri ya kuishi na ustawi, idadi kubwa ya uzalishaji wa kaboni inatishia hatma ya watoto wote, ripoti hiyo imegundua.

Aidha ripoti imeongeza zaidi kwamba hakuna nchi moja iliyofanya vizuri kwenye hatua zote tatu za ukuaji wa maendeleo ya watoto, ustawi, na usawa.

Ripoti hiyo pia ilionyesha vitisho kwa watoto vilivyotokana na sekta ya biashara. Utazamaji wa matangazo ya vyakula visivyo na afya na vyenye mafuta na sukari vimehusishwa na unene uliopitiliza wa watoto.

Watoto pia huonyeshwa matangazo ya bidhaa yaliyokusudiwa watu wazima, kama vile pombe na tumbaku, na kuongeza nafasi ya utumiaji.