Machafuko nchini Nigeria, 300 wameshakufa.
30 Julai 2009Matangazo
MAIDUGURI.
Polisi nchini Nigeria imesema watu zaidi ya 300 wameshauawa kutokana na mapambano ya siku nne baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la kiislamu, kaskazini mwa Nigeria.Maalfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mapigano hayo.
Maafisa wa serikali wamesema mapigano hayo yapo hasa katika mji wa Maiduguri, ambao ni makao ya kundi hilo linaloiga mfano wa taliban. Kundi hilo linapigania kutumiwa kwa sheria za kiislamu nchini Nigeria kote.
Rais Umaru Yar'Adua ameliagiza jeshi kuwazima waislamu hao mara moja.