SiasaUfaransa
Macron akabiliwa na upinzani zaidi nchini mwake
17 Machi 2023Matangazo
Kwa kutumia mamlaka maalum ya kikatiba kupitisha sheria bila kura ya bunge, iliashiria kukiri kuwa serikali haina wingi wa kura katika uamuzi wa kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64, mabadiliko ambayo yamekumbwa na upinzani mkali kote nchini humo. Baraza la Seneti liliidhinisha mswada huo mapema jana, lakini kusitasita kwa wabunge wa upinzani wenye siasa za mrengo wa kulia kumuunga mkono Macron, kulimaanisha kuwa serikali ingeshindwa kuupitisha mswada huo bungeni. Usafiri wa treni, masomo shuleni, huduma za umma na bandarini tangu Januari zimeathirika na migomo ya kupinga mageuzi hayo, wakati kukiwa na maandamano makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miongo mingi.