Macron asikitishwa na Ufaransa kutokuzuwia mauaji ya Rwanda
5 Aprili 2024Matangazo
Afisa mmoja wa Ofisi ya Rais wa Ufafransa ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina alisema katika video inayotarajiwa kusambazwa siku ya Jumapili kukumbuka miaka 30 ya mauwaji ya halaiki ya Rwanda, Rais Macron atasisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa ilikuwa na njia ya kujuwa na kuchukuwa hatua za kuzuwia mauwaji hayo, na ingelifanya hivyo kama ingelitaka.
Soma zaidi: Macron akiri Ufaransa ingeliweza kuzuwia mauaji Rwanda 1994
Hata hivyo, Macron hatahudhuria maadhimisho ya mauaji ya kimbari Jumapili ya tarehe 7 mjini Kigali, Rwanda, na badala yake Ufaransa itawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Stephane Sejourne.