MigogoroUkraine
Macron: Hatujaondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi Ukraine
27 Februari 2024Matangazo
Rais Emmanuel Macron amekataa kutoa maelezo juu ya mataifa ambayo yanafikiria kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine.
Macron amewambia viongozi waliokusanyika mjini Paris kwamba watafanya kila linalowezekana kuizuia Urusi kushinda vita hivyo ambavyo vimeingia mwaka wake wa tatu sasa.
Rais huyo wa Ufaransa amewahimiza viongozi wa Ulaya kuhakikisha kile alichokiita "usalama wa pamoja" wa Ulaya kwa kuiunga mkono Ukraine hasa wakati huu ambapo inakabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi.
Mkutano huo umehudhuriwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Poland Andrzej Duda pamoja na viongozi kutoka ukanda wa Baltic.