Macron kutumia kifungu cha katiba kuptisha mfumo wa pensheni
16 Machi 2023Matangazo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameamua kulazimisha kuuidhinisha mpango wake wa mageuzi ya pensheni bila kuitisha kura bungeni.
Maandamano mapya kuhusu muswada wa pensheni Ufaransa
Vyanzo kadhaa vilivyo karibu na ofisi ya rais vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kiongozi huyo atatumia uwezo wa kikatiba unaoiwezesha serikali kuwapiku wabunge.
Rais Macron amechagua kukitumia kifungu cha 49.3 cha katiba ya Ufaransa baada ya mikutano kadhaa na viongozi wakuu, akiwemo Waziri Mkuu Elisabeth Borne, baada ya kubaini kwamba hakukuwepo na wabunge wengi wa kupitisha mageuzi hayo.