1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Francophonie

4 Oktoba 2024

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa atakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa siku mbili wa Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa (Francophonie) akitumai kuimarisha ushawishi wa nchi hiyo hususani barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4lQGz
Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.Picha: Djordje Kojadinovic/REUTERS

Mkutano huo wa Jumuiya ya Francophonie yenye nchi wanachama 88 unafunguliwa leo na utaendelea hadi kesho Jumamosi na unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka 33. 

Macron anawakaribisha viongozi hao wakatii kukiwa na msukusuko unaouandama utawala wake tangu kumalizika kwa uchaguzi wa bunge wa majira ya kiangazi, ambao chama chake kilishindwa kupata wingi wa viti kuunda serikali. 

Soma zaidi: Vijana wa Afrika kupewa kipaumbele asema Macron

Kadhalika ushawishi wa Ufaransa barani Afrika umetetereka kutokana na mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Niger yaliyoziangusha tawala zilizokuwa na usuhuba na serikali mjini Paris.