1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madaktari wasema watu 22 waliuawa wakati wa maandamano Kenya

26 Juni 2024

Chama cha madaktari nchini Kenya kimesema takriban watu 23 waliuawa na wengine 30 wanapokea matibabu kutokana na majeraha ya risasi walioyapata wakati wa maandamano ya kupinga ongezeko la ushuru.

https://p.dw.com/p/4hXwg
Kenya | Nairobi
Polisi nchini Kenya ikijaribu kuwadhibiti waandamanaji Picha: Gerald Anderson/Anadolu/picture alliance

Rais wa chama hicho Simon Kigondu amesema hajawahi kuona kiwango cha aina hiyo ya vurugu dhidi ya watu wasio na silaha.

Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu linalofadhiliwa na serikali KNHCR limeahidi kufanya uchunguzi juu ya kile ilichoeleza kuwa “idadi kubwa ya vifo kutokea katika siku moja ya maandamano.”

Rais wa Kenya aukataa muswada wa fedha 2024

Mwenyekiti wa shirika hilo Roseline Odede ameongeza kuwa, 19 kati ya hao 23 waliuawa mjini Nairobi.

Ameeleza kuwa shirika hilo limeorodesha zaidi ya watu 300 waliojeruhiwa na wengine zaidi ya 50 waliokamatwa.
 

Vurumai ya waandamanaji vijana yautikisa mji mkuu wa Kenya