1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana nchini Kenya kuipinga serikali

27 Machi 2023

Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Kenya Nairobi licha ya tamko la serikali kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4PJnF
Proteste in Kenia
Picha: Ben Curtis/AP/dpa/picture alliance

Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wandaamanaji hao.

Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, aliungana na waandamanaji huko magharibi mwa jiji la Nairobi ambapo msafara wake uliwavuta maelfu ya wafuasi.

Odinga alitoa hotuba wakati wa maandamano hayo na kutaka haki ya uchaguzi na kupunguza bei za vyakula.

Mkuu wa Polisi nchini Kenya Inspekta Jenerali Japheth Koome amesisitiza kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria lakini Odinga amesema Wakenya wana haki ya kuandamana.