Maelfu waathiriwa na mafuriko mashariki mwa Kongo
20 Aprili 2024Msemaji wa mamlaka ya mji wa Uvira Dominique Kalonzo amesema, takriban nyumba 4,500 zimebomoka, zaidi ya viwanja 2,000 vikifunikwa na maji huku zaidi ya kaya 7,000 pamoja na shule 53 zikiathiriwa kutokana na mito iliofurika na kuongezeka kwa kina cha maji ziwa Tanganyika.
Msemaji huyo ameongeza kwamba wakaazi walioathirika wamejihifadhi kwa ndugu na jamaa huku wengine wakilala nje licha ya hali mbaya ya hewa, huku akisisitiza kuwa halmashauri ya mji imeomba msaada wa dharurakwa serikali kuu na mashirika ya kiraia kutokana na mji kukabiliwa na hatari ya kukumbwa na magonjwa.
Soma pia:Burundi yahitaji msaada kukabiliana na mafuriko makubwa
Mbali na Kongo eneo la Afrika mashariki linakumbwa na mvua kubwa iliosababisha vifo vya watu 58 nchini Tanzania katika wiki mbili za kwanza za mwezi Aprili na wengine 32 hivi karibuni nchini Kenya.