JangaMarekani
Maelfu watakiwa kuhama baada ya moto mpya kuzuka Marekani
23 Januari 2025Matangazo
Moto huo uliopewa jina la Hughes Fire, unawaka karibu na eneo maarufu la burudani karibu na Ziwa Castaic, kama kilomita 64 kutoka eneo kulikowaka moto mkubwa kabisa, ambao bado haujazimwa kikamilifu tangu ulipozuka Januari 7.
Soma pia: Waliofariki katika moto wa nyika Los Angeles wafikia 16
Mkuu wa polisi katika kaunti ya Los Angeles Robert Luna amesema zaidi ya watu 31,000 wameagizwa kuondoka hadi sasa.
Amesema, "Na hivi sasa, idadi niliyonayo ni kwamba kuna takriban watu 31,000 ambao watatakiwa kuhama. Wengine 23,000 pia wataathirika kufuatia maonyo haya ya kuhama."
Bado haijajulikana ikiwa kuna mali zilizoharibiwa na moto huo mpya.