Madaktari waandamana Ujerumani kupigania hali njema kwao
12 Machi 2024Matangazo
Monika Heinold, mpatanishi mkuu wa waajiri amesema yapo matumani ya kufanyika mazungumzo zaidi. Madaktari hao wanadai nyongeza ya mishahara ya asilima 12.5 pamoja na marupurupu ya juu kwa kazi za kawaida za nyakati za usiku, mwishoni mwa juma na likizo za umma.
Kwa mujibu wa chama cha madaktari, Marburger Bund, takriban madaktari 7,000 kutoka hospitali 23 za vyuo vikuu walishiriki maandamano hayo. Awamu ya nne ya mazungumzo kati ya chama cha madaktari na waajiri ambao ni majimbo ya shirikisho ya Ujerumani hayakuwa na matokeo chanya.