MigogoroUingereza
Maelfu ya polisi waandaliwa kukabili vurugu Uingereza
7 Agosti 2024Matangazo
Machafuko yalizuka baada ya watoto watatu kuuawa wiki tatu zilizopita. Makundi ya mrengo mkali wa kulia yamepanga kufanya maandamano kwenye maeneo zaidi ya 30 kuzilenga sehemu zinazowahifadhi wakimbizi.
Serikali imesema imewaweka tayari polisi maalumu 6,000 ili kupambana na ghasia ambazo hazijawahi kushuhudiwa nchini Uingereza katika muda wa miaka 10 iliyopita.
Mamia ya watu wamekamatwa na wengine zaidi ya 100 wamefunguliwa mashtaka.
Waziri Mkuu Keir Starmer ametoa onyo kwa wote watakaohusika kwamba watauona mkono thabiti wa sheria ikiwa pamoja na wale wanaochochea fujo kwenye mitandao.