Maelfu ya wanajeshi wajiunga kwenye luteka za NATO
18 Juni 2024Matangazo
Karibu wanajeshi 9,000 kutoka mataifa 20 wanachama wa Jumuiya ya NATO wanashiriki kwenye luteka za kijeshi mwezi huu katika ukanda wa Bahari wa Baltiki, ambao umekuwa eneo tete la kimkakati tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.
Sweden iliyowahi kufanya luteka hizo huko nyuma, ilishiriki kwenye luteka ya Baltops kwa mara ya kwanza mwezi Juni kama mwanachama kamili wa NATO baada ya kujiunga mapema mwaka huu.
Luteka hizo zilizohusisha vikosi vya maji, anga na ardhini zimekuwa zikifanyika katika Bahari ya Baltiki pamoja na Sweden na kisiwa chake cha kimkakati cha Gorland, Lithuania, Poland na Ujerumani.
Zitafanyika hadi Alhamisi na kuhusisha manowari 50 za kivita na ndege 45 za kijeshi pamoja na helikopta.