1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamana Karabakh kudai kufungua barabara ya Armenia

14 Julai 2023

Maelfu ya watu wameandamana leo katika mkoa wa Nagorno-Karabakh nchini Azerbaijan, wakiitaka serikali ya Baku iikifungue barabara pekee inayoiunganisha eneo hilo na Armenia.

https://p.dw.com/p/4Ttik
Armenien Proteste vor russischem Militärstützpunkt Nr. 102
Picha: Alexander Patrin/Tass/dpa/picture alliance

Karabakh imekuwa kitovu cha mgogoro wa miongo kadhaa ya umiliki kati ya Azerbaijan na Armenia, ambazo zimepigana vita mara mbili vya udhibiti wa eneo hilo la milima, ambalo lina wakaazi wengi wa Kiarmenia.

Jumanne wiki hii, Azerbaijan ilisema inaifunga kwa muda barabara kuu ya Lachin, ikilituhumu tawi la Armenia la Msalaba Mwekundu kwa ulanguzi.

Hatua hiyo ilizusha wasiwasi wa kuzuka mzozo wa kibinaadamu katika mkoa huo, ambao unakumbwa na uhaba wa chakula na ambako wenyeji wanakosa huduma za afya.

Karibu watu 6,000 wameandamana leo katika mji mkuu wa Karabakh, Stepanakert.