1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sayansi

Maelfu ya watu wahamishwa kutoka eneo la volkano Ufilipino

11 Juni 2023

Maelfu ya watu wanaoishi eneo la volkano nchini Ufilipino wamepewa hifadhi katika vituo vya uokoaji wakati maafisa wakionya leo kuhusu hatari ya kiafya kutokana na jivu na gesi za sumu zinazofuka kutoka Mlima Mayon.

https://p.dw.com/p/4SRXe
Philippinen | Vulkan Mayon
Picha: John Michael Magdasoc/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya ulinzi wa raia ya Ufilipino imesema zaidi ya watu 12,800 wamehamishiwa vituo vya uokoaji, wengi wao kutoka vijiji vya wakulima vilivyoko kwenye eneo la volkano.

Watafiti wa matetemeko ya ardhi wamesema walirekodi tetemeko moja la volkano katika saa 24 zilizopita na miamba yenye moto inaanguka kutoka Mlima Mayon unaopatikana katika mkoa wa kati wa Albay.

Mayon iko umbali wa kilomita 330 kusini mwa mji mkuu, Manila, na inazingatiwa kuwa mojawapo ya milima 24 nchini humo yenye hatari kubwa zaidi ya kutokea volkano.