1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiCanada

Maelfu ya watu watoroka makwao Canada kufuatia moto

30 Mei 2023

Zaidi ya watu 16,000 wamelazimika kuhama makwao huku shule zikifungwa katika mkoa wa mashariki mwa Nova Scotia nchini Canada kufuatia moto mkali unaoendelea kuwaka.

https://p.dw.com/p/4RxOT
Kanada | Waldbrände
Picha: B.C. Wildfire Service/Handout/REUTERS

Picha za televisheni zimeonyesha moshi mkubwa huku nyumba kadhaa na magari yakiteketezwa na moto huo japo hakuna majeruhi yoyote yaliyoripotiwa.

Moto huo ambao bado unawaka bila ya kudhibitiwa  kwenye viunga vya kaskazini magharibi mwa mji wa Halifax, haujasambaa sana tangu hali ya hatari ilipotangazwa Jumapili jioni japo imewalazimu wakaazi wa mji huo kuondoka.

Gavana wa jimbo la Nova Scotia Tim Houston amesema wakaazi wa jimbo hilo wanaishi kwa wasiwasi wakati meya wa Halifax Mike Savage akisema mji huo wenye wakaazi 430,000 wanakabiliwa na hatari ya kutokea moto wakati wowote.

Kuanzia jana, moto umezuka katika mikoa nane kati ya 13 nchini Canada.