1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafashisti mamboleo NSU, mahakamani

Abdu Said Mtullya7 Mei 2013

Wahariri wanazungumzia juu ya kesi kubwa inayowakabili mafashisti mamboleo wa Ujerumani, na juu ya mgogoro wa Syria.

https://p.dw.com/p/18TVz
Mafashisti mamboleo wafikishwa mahakamani
Mafashisti mamboleo wafikishwa mahakamaniPicha: DW/S Sokollu

Kuhusu kesi inayowakabili mafashisti mamboleo wa Ujerumani gazeti la "Der neue Tag"linasem walioathirika na mauaji yaliyofanywa na mafashisti mamboleo  wanataka haki itendeke. Mhariri wa gazeti hilo anasema watu hao wanataka kila hatua ichunguzwe. Ni kwa njia hiyo tu kwamba majonzi yao  yatapungua.

Gazeti la "Saarbrücker" linasema  licha ya kesi hiyo kuahirishwa, baada ya kuanza hapo jana, bado ni hatua ya ushindi kwa ndugu na jamaa wa wale waliouawa. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba kuahirishwa kwa kesi hiyo hakutabadilisha ukweli kwamba siku ya jana ambapo kesi ilisikilizwa, ilikuwa ya ushindi kwa haki.

Gazeti linaeleza kuwa baada ya miaka yote ya majonzi,tashwishi na tuhuma,sasa umefika wakati wa msema kweli.Na "tunatumai hatima yake utakuwa wasaa wa haki."

Lakini mhariri wa "Lauzitser  Rundschau" anatahadharisha juu ya kuweka  matumaini ya juu sana kuhusu kesi inayowakabili mafashisti mamboleo watano  wanaokabiliwa na mashtaka ya kuwaua watu kadhaa kwa sababu za kibaguzi. 

Anasema katika miezi inayofuatia itaonekana iwapo kesi hiyo itaendelea na kuweza kufikia hukumu, baada ya mahakama yenyewe kujitatanisha. Itakuwa vigumu lakini ni jambo linalowezekana ikiwa matarajio na maswali ya ndugu wa waliouawa yatazingatiwa. Naye mhariri wa "Badische  Neueste Nachrichten" anasema itachukua miaka kadhaa hadi kutolewa hukumu. Hadi wakati huo busara itatawala licha ya kiwango cha uhalifu uliotendeka.

Mgogoro wa Syria:
 Wahariri wa magazeti pia wanataoa maoni juu ya mgogoro Syria,kuhusiana na uchunguzi juu ya silaha za sumu- iwapo zimetumika au la. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Carla del Ponte amesema pana dalili kwamba silaha hizo zilitumiwa na wapinzani. Juu ya madai hayo gazeti la "Landeszeitung" linasema:

Carla del Ponte anaupalia makaa mgogoro wa Syria kwa kuyatoa madai hayo.Hata hivyo anastahiki kutiliwa maanani. Gazeti  linasema ni kweli kwamba hawezi kuyathibitisha madai anayoyatoa kuwa wapinzani yumkini walizitumia silaha za sumu. Lakini mashirika ya ujasusi ya nchi za magharibi pia hayawezi kuthibitisha  iwapo majeshi ya serikali ya Syria yaliitumia gesi ya sumu.

Hata hivyo mjumbe wa Umoja wa Mataifa del Ponte ,angalau ameweza kuuvunja  mwiko katika mtazamo ambao umekuwa unashikiliwa na nchi za magharibi, kwamba waasi, kwa kutumia mbinu za uhalifu wa kivita, na kumsingizia Rais Assad, wangeliweza kuziingiza nchi za magharibi katika vita vya nchini Syria.

Mwandishi:Mtullya  Abdu./Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman