Mafuriko, maporomoko yasomba nyumba kadhaa Kenya
30 Aprili 2024Matangazo
Awali afisa mmoja wa polisi katika eneo hilo, Stephen Kirui, alikuwa ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba bwawa la Kijabe lililoko katika eneo hilo la Mahi-Mahiu lilivunja kingo zake na kubeba matope, mawe na pia kung'oa miti.
Soma zaidi: Bwawa lapasua kingo Kenya, watu 45 wapoteza maisha
Lakini katika taarifa iliyotolewa jana jioni, serikali ya Kaunti ya Nakuru ilisema kuwa mafuriko hayo yalitokana na kuziba kwa njia ya reli.
Magari yalikwama kwenye tope hizo huku wahudumu wa afya wakiwatibu waliojeruhiwa wakati maji hayo ya mafuriko yakiendelea kufunika maeneo mengine.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa watu 109 wamelazwa hospitalini huku wengine 49 wakiwa hawajulikani walipo.