Mafuriko yawaathiri watu 760,000 Sudan Kusini
4 Novemba 2021Matangazo
Ofisi hiyo imesema majimbo manane kati ya kumi yamekumbwa na mafuriko nchini Sudan Kusini, ambayo yanaathiri huduma za afya na huduma nyenginezo.
Juhudi za misaada zimekuwa zikitanzwa na mapigano kati ya makundi ya kikabila kusini mwa nchi hiyo, na watu kadhaa kukimbilia Uganda.
Mwezi uliopita, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, liliyaelezea mafuriko hayo kuwa mabaya kabisa kuwahi kutokea kwenye baadhi ya maeneo tangu mwaka 1962, likisema yamesababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Mafuriko ya sasa yalitanguliwa na mvua iliyonyesha kwa miezi sita mfululizo, na hivyo kuathiri uwezo wa watu kukabiliana na athari zake.