1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazeti ya Ujerumani hii leo yanazungumzia mkutano wa chama cha kijani.

S.Kitojo4 Desemba 2006

Mkutano wa chama cha Kijani, Greens, cha Ujerumani, baada ya kumalizika mwaka mmoja wa utawala wa serikali ya muungano ya chama cha SPD na CDU, ndio mada kuu katika magazeti ya Ujerumani hii leo. Hususan yametupia macho mwelekeo wa uwezo wake wa kuwa chama kinachoweza kuunda serikali ya mseto. Pamoja nanyi katika magazeti hii leo ni Sekione Kitojo.

https://p.dw.com/p/CHUI
Wanachama wa chama cha kijani wakitafuta mwelekeo wa chama chao.
Wanachama wa chama cha kijani wakitafuta mwelekeo wa chama chao.Picha: AP

Mwaka mmoja baada ya kuanguka kutoka madarakani katika serikali ya Ujerumani chama hiki kinachopambana kuwa na hali bora ya mazingira kimetambua wazi kuwa hatimaye kimekuwa chama cha upinzani. Linaandika gazeti la Westlälischen Nachrichten kutoka Münster.

Kuhusu suala hili la madaraka , chama hiki hakitaki kuachana nalo. Chama hiki bila ya kuwa na kiongozi wao mwenye heba Joschka Fischer kinaonekana kwa kiasi kikubwa bila shaka kinataka kufanya mabadiliko.

Mkutano wa chama hicho uliofanyika mjini Kolon mwishoni mwa Juma umeweza kutoa mwelekea na hali bora katika makao yake makuu.

Iko haja ya kuweka sawa suala la mazingira, ama kibaki kuwa chama kinachoweza kuunda muungano katika serikali na kutowatisha wapiga kura kutoka katika mwelekeo tofauti.

Katika gazeti la Stuttgater Nachrichten tunasoma.

Kama uwezekano mwingine wa serikali ya mseto inaonekana hivi sasa kuelekeza katika serikali ya mseto ya muungano mkubwa zaidi wa vyama vitatu.

Katika hali hiyo chama cha Kijani kinaweza kuwa chama shirika siku zijazo.Lakini kwa muda mrefu hawajakuwa na nia , ili kuwaweka mbali vyama vingine ambavyo vina uwezo wa kufanya hivyo.

Gazeti la Nordbayerische kutoka Bayreuth linadokeza kuwa.

Ndio kulikuwa na wakati baada ya Joschker Fischer, lakini chama cha Kijani kimejiletea wakati huo huo katika mabunge kadha ya majimbo na la shirikisho upinzani mkubwa. Katika hilo kuna nafasi ya chama hicho cha kijani kupambana kufanya mageuzi. Chama cha kijani kinatambua kuwa nafasi yake inakuja. Wakati muungano mkubwa wa serikali ukimaliza muda wake , baadaye mwaka 2009, chama hicho kinaweza kuwa na chama cha SPD, na hata pengine katika vyama ndugu vya CDU na CSU. Huenda chama cha kijani kikahitaji mshirika wa kuunda nae serikali.

Nalo gazeti la Leipziger Volkszeitung linaandika kuwa.

Kwa chama cha SPD , chama cha Kijani kilikuwa si kitu kingine mbali ya chama cha kutoa msaada tu kwake. Kwa vyama ndugu vya CDU na CSU , chama cha kiliberali cha FDP kinakiona chama cha kijani kuwa ni chama ambacho hakikuwa na usemi katika utawala uliopita serikali.

Lakini kwa upande wa magazeti ya Essen ya Neue Ruhr na Neue Rhein Zeitung yanapinga maoni hayo.

Magazeti hayo yanaandika kuwa chama cha kijani kiko katika upinzani katika mabunge yote, ya majimbo na shirikisho.

Kinataka kuangalia nafasi zote. Kina mawazo tele, mchanganyiko wa jamii mbali mbali, kinasifa ya kuwa na jeuri ya chama , chenye msimamo mkali, lakini sio katika nadharia za ghasia, badala yake katika suala la kutoyumba, yenye mwelekeo na bila kurudi nyuma. Chama hiki kinalenga katika mwelekeo wa kulinda mazingira. Lakini changamoto hii inatambulika kwa muda mrefu na vyama vyote.

Na gazeti la Berliner Tagesspiegel linadokeza kuwa:

Mwaka mmoja ndio umemalizika katika utawala wa serikali ya mseto baina ya chama cha SPD na CDU, chama cha kijani kimeonyesha mwishoni mwa juma kuwa chama hicho kiko mbali na mwelekeo wazi. Uongozi wa chama hicho unageuza macho upande wa kushoto huku ukitaka kwenda mbele, na hivyo kutoweza kutoa mwelekeo maalum. Msingi wa chama hicho ungependelea zaidi kuelemea upande wa shoto, lakini kinashindwa kupata njia.