Magazetini: Boris Johnson madarakani mtaa wa Downing
24 Julai 2019
Tukianza na gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung , mhariri anaandika kwamba itakuwaje pale mtu huyu mtu katika ofisi ya waziri mkuu ya mtaa wa Downing namba 10 atakavyokuwa mara akitambua ugumu wa majukumu yake, hususan atakapoanza kuona uzito wa uwajibikaji. Mhariri anaandika:
"Mzozo wa Uingereza na Iran, unaonesha kile kitakachotokea kwa Boris Johnson. Umoja wa Ulaya unaonesha uvumilivu dhidi ya uchokozi unaofanyiwa mwanachama wake, dunia lakini haisubiri, hadi pale wanasiasa wa Uingereza watakapouzima. Ni kwa kiasi gani uhusiano katika ya Uingereza na Ulaya utakuwa wa karibu, na ni ukaribu wa kiasi gani mwanasiasa huyu Johnson atajongeleana na rais wa Marekani. Trump amempaka mafuta mara kadhaa, na kwa hiyo Johnson hapaswi kulewa na sifa hizo. Kwa upande wao mataifa ya Ulaya yanamuhitaji , kadiri ya inavyowezekana, kumnyooshea mkono, lakini si bila shaka kutafuta kuitumbukiza Uingereza shimoni."
Nae mhariri wa gazeti la Stuttgarter Zeitung akindika kuhusu kuingia madarakani kwa Boris Johnson anasema:
"Johnson anakalia kuti kavu katika madaraka yake. Wingi katika bunge ni mwembamba mno, anaweza wakati wowote kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nae bungeni. Na wengi wa wabunge wanapinga makubaliano ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya Brexit bila ya kupata makubaliano. haujaondoka uwezekano , kwamba badala ya Brexit kunaweza kuwa na uchaguzi mpya nchini Uingereza na kura ya pili ya maoni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kutokana na matokeo ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya."
Mhariri wa gazeti la Leipziger Volkszeitung , nae anaandika kuhusu kuingia madarakani kwa Boris Johnson nchini Uingereza. Mhariri anasema:
"Katika siku ya kwanza tu katika ofisi ya mtaa wa Downing Johnson atatambua, kwamba sio tu Brexit , badala yake suala la Iran ndio mada muhimu zaidi inayomsubiri. Katika mzozo na Iran wanadiplomasia wa Uingereza, wanataka haraka kuweka umoja katika Umoja wa Ulaya kuunda ujumbe wa kikosi cha kulinda mlango bahari wa Hormuz. London inataka kwa hiyo , kuwa karibu na Umoja wa Ulaya. Mhariri hata hivyo anauliza , ni vipi inawezekana kwenda pamoja na wanasiasa wa Uingereza , wakati lengo la wanasiasa hao ni kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya."