Magazetini: Mkutano Trump na Putin na EU na Japan na China
17 Julai 2018Mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung akiandika kuhusu mkutano kati ya Donald Trump na Vladimir Putin anasema kwamba ni vizuri Marekani na Urusi zinafanya majadiliano baina yao, kuliko kwamba wanafanya tu mazungumzo. Mhariri anaendelea:
"Hadi sasa kuna habari nzuri kwamba mkutano wao huo mjini Helsinki hatimaye ulifanyika. Undani wa mazungumzo yao lakini pamoja na matokeo yake bado yamo katika ukungu. Mkutano wa kilele, ni mzuri kama unavyoonekana, lakini hauondoa mizozo ya baadaye."
Mjini Helsinki hakukuwapo na maazimio kamili, kulikuwa na viongozi wawili wa kitaifa walioshikana mikono, na pia kuhakikisha kwamba wanaweza kukutana tena. Anaandika hivyo mhariri wa gazeti la Mannheimer Morgen kuhusu mkutano kati ya Trump na Putin. Mhariri anaandika:
"Hii inapendeza katika hatua za mwanzo, katika kufanya bora mahusiano baina ya Marekani na Urusi. Kwa mtazamo wa Ulaya lakini huu ni mwanzo wa ushirikiano tete, ushirikiano ambao una lengo na maslahi ya binafsi. Ni mwanzo wa kukwepa maadili yanayowakilisha Ulaya. Hakuna mtazamo unaoweza kuleta utulivu."
Mhariri wa gazeti la Freie Presse la mjini Chemnitz anaandika kuhusu mkutano huo kati ya Trump na Putin kwa kusema, kwamba kwa Putin mkutano huo ulikuwa kiki ya kujitangaza. Mhariri anaendelea:
"Kwanza mashindano yaliyokuwa na mafanikio ya kombe la dunia nchini Urusi, kisha mkutano na nchi yenye nguvu duniani katika kiwango sawa ana kwa ana. Hakuna kitu bora kilichowahi kumtokea Putin katika siku hizi kuliko ilivyokuwa. Kitu halisi kilichotokea katika mkutano huo wa kilele? hiyo itakuwa kazi kwa ajili ya uchambuzi wa kina."
Mada nyingine inahusu mkutano wa kilele wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya, China na Japan. Mhariri wa gazeti la Die Welt la mjini Berlin anaandika kwamba kutokana na wasiwasi wa kuporomoka kwa haraka kwa uhusiano kati ya Putin na Trump, katika kivuli cha mzozo wa kibiashara duniani kuna kitu kipya ghafla kinamea. Mhariri anaandika:
"Ushahidi ni kwamba inaelekea kuna mabadiliko ya uhusiano wa mataifa yenye nguvu duniani. Ghafla China imeonesha utayari wa kufanya majadiliano katika masuala ya biashara na kutangaza kwamba inataka kuwekeza katika mataifa ya Ulaya. Na pia Japan na mataifa ya Ulaya yanajongelea kwa kiasi kikubwa. Anataka Trump kuhatarisha pia TPP na Nafta, ukaribioano baina ya Umoja wa Ulaya na washirika wake hao wawili muhimu wa kibiashara katika eneo la mashariki ya mbali unaonekana."
Mada ya mwisho ni kuhusu mzozo katika mashariki ya kati, mhariri wa gazeti la Suedwest Presse la mjini Ulm anaandika:
"Ndege za kivita za Israel zimelishambulia eneo la kaskazini, ikiwa ni jaribio la kuondoa uwezekano wa kushambuliwa upande wa kusini, ambako vikosi vya jeshi la Syria na washirika wake wanakaribia kwa kilometa chache kabisa mpaka wake. Kwa Israel kusongambele kwa Iran ama hata jaribio lake, la kubakia kwa muda mrefu nchini Syria , ni sababu ya vita. Kuimarika kwa jukumu la Iran katika nchi hiyo jirani ya Israel ni kitisho kwa uhai wa nchi hiyo."
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Josephat Charo