Magazetini: Mpango mbadala wa May wa Brexit
31 Januari 2019Tukianza na mada kuhusu mpango mbadala wa waziri mkuu wa Uingereza Theresa May katika Brexit, mhariri wa gazeti la Rhein-Zeitung anandika:
"Mbinu za majadiliano za Uingereza hazionekani kuwa na mipango sahihi. Hali hiyo imeonekana kwa muda mrefu sasa, na haijaondoka. Makampuni ya kuunda magari, tasinia ya filamu, makampuni ya kutengeneza madawa, hakuna kinachokwenda, kwa kuwa wanasubiri kuidhinishwa kwa mpango wa Brexit mwezi wa Februari, na inaonekana kuwa katika kipindi kijacho hakutakuwa na suluhisho kwa kuwa kuna baadhi ya wanasiasa nchini humo ambao wanamuonesha waziri mkuu kuwa hafai badala ya kuangalia hali ya baadaye ya nchi yao."
Mhariri wa gazeti la Mannheimer anaandika kuhusu Brexit kwa kusema kwamba suala la hali tete ya Ireland ya kaskazini kwa wanasiasa wengi lilionekana kuwa si kitisho. Mhariri anaendelea:
"Hali hiyo inatia wasi wasi na kushitua , ikiwa ushahidi lakini pia ni kwamba serikali ya Uingereza haitaki kupata kuaminika, kutokana na suala hilo la eneo la Ireland ya kaskazini. Kwa hiyo basi Umoja wa Ulaya unataka kuhakikisha maslahi ya watu wa Ireland yanalindwa. Suala la mpaka halina mjadala, na pia lisiwe suala litakalotumiwa kufanya harakati za kisiasa za chama cha waziri mkuu."
Waziri wa ulinzi
Kuhusiana na mada juu ya jeshi la Ujerumani kupata vifaa muhimu vya kutendea kazi, gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika:
"Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen , alipoingia madarakani alijaribu kuweka mambo sawa katika wizara hiyo, lakini sasa inaonekana kwamba hata yeye binafsi yuko gizani. Masuala ya kupanda kupita kiasi gharama za meli ya mafunzo, ya Gorch Fock, na mengineyo katika jeshi la Ujerumani , na washauri wa nje wa wizara kushindwa kutoa tahadhari na mapema yanaonesha wazi kwamba jaribio la Von der Leyen kuweka kando mara kwa mara mpango wa kulipatia vifaa jeshi ni wazi kabisa kwamba mambo mengi hayaendi sawa na si rahisi tena."
Gazeti la Reutlinger General - Anzeiger likizungumzia kuhusu kuzuwia shambulio la kigaidi , linaandika:
"Kitisho kwa jamii ya Ujerumani ni mipango ile ya mashambulizi kuweza kuzuwia kwa wakati muafaka kabla ya utekelezaji wake, kwa sababu hali hiyo inachafua utulivu wa jamii na kusababisha watu kutoa hukumu ya kabla. Hususan kwa wakimbizi , wanaonekana kuwa kuna uwezekano wa wao kufanya shambulio la kigaidi kuliko kwamba hawa ni watu wanohitaji msaada na kulindwa. Hali hii inawapa fursa wale wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia ya kuonesha chuki yao dhidi ya wageni. Kinachoshangaza hiyo ndio nadharia ya mafanikio ya kundi kama la IS, ili kupambana na kile inachokiita mfumo wa mataifa ya magharibi, wa kiliberali na mfumo unaotambua haja ya kuishi pamoja licha ya kutengana kimawazo."
Mwandishi: Sekione Kitojo / ilandspresse
Mhariri: Idd Ismail Ssessanga