Magazetini: Uhuru wa vyombo vya habari
3 Mei 2018Gazeti la Badische Zeitung la mjini Freiburg katika siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari linaandika:
Uhuru wa vyombo vya habari unaingia katika kila kitu. Kila mahali. Ni haki isiyoweza kuwekwa katika mjadala na ni sehemu ya uhuru wa kutoa maoni na demokrasia. Kwanza kabisa vyombo vya habari vilivyo huru vinawezesha jamii kuwa huru. Pale ambapo hakuna , kuna uwezekano kwa wenye madaraka kutumia hali hiyo kufungua milango ya kutumia vibaya madaraka yao. Kuyaona haya sio tu China na Korea kaskazini.
Hata nchini Uturuki kumekuwa na hali ya ukandamizaji dhidi ya waandishi habari na kubanwa kwa haki za kiraia. Nchini Hungary ama hata Poland hali ya vyombo vya habari vya binafsi ni mbaya na vinatakiwa kufuata muongozo wa vyombo vya serikali. Katika hali hiyo kitisho cha uhuru wa vyombo vya habari si tu kwamba ni kikubwa, lakini maafisa, wanajaribu kuwatumia waandishi kuandika kile wanachotaka ili kujenga ukuta, na kuwatumia wadau wa habari, pamoja na wagombea wa kiti cha meya na kuondoa uhuru wa vyombo vya habari kama tunavyouelewa leo hii na kuondoa kuaminika kwao.
Kuna dawa lakini kwa hili. Ni kuwa wakweli katika uandishi habari. Sio kutofanya makosa , lakini kuwa wakweli kuhusiana na mapambano ya kupata taarifa muhimu.
Gazeti la Die Welt linaandika kuhusu siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari. Mhariri anaandika:
Katika bahari ya dunia ya kutovumiliana na hali inayoongezeka ya kubanwa kwa uhuru wa raia Ujerumani ni kisiwa kilichobarikiwa. hata hivyo ni lazima tunalazimika kuangalia kwa kina , kazi za waandishi habari ama vyombo vya habari kwa ujumla vinapata vizuwizi ama kushindwa kufanya jambo.
Hii pia inahusika katika mjadala ambao hivi sasa unafanyika kuhusiana na jukumu la huduma za utangazaji halali kwa umma na kuna nafasi gani kwa vyombo vya habari vinavyopata fedha kutoka vyanzo vya binafsi katika uchumi wa nchi. Matamanio makubwa ya uhuru nchini Marekani ni muhimu kwa wadau wa uhuru wa vyombo vya habari hapa Ujerumani kuutilia maanani.Hakuna mtu mwenye uhakika kuhusiana na adui wa ndani. Uhuru wa vyombo vya habari ni lazima kila siku uelezewe upya. Kutokuwa na uhuru ni hali bila shaka iliyopo duniani kote, lakini mara nyingine hata kwetu hali hiyo ipo.
Nalo gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, linazungumzia sera ya bajeti , mhariri anaandika:
Angalia hesabu, unakosa kuona, licha ya changamoto za wahamiaji, kidigitali, mabadiliko ya tabia nchi na uchokozi duniani Umoja wa Ulaya na pia Ujerumani zinataka kuyaweka mambo hayo katika wakati uliopita.
Licha ya kujitoa Uingereza , nchi ya pili inayochangia katika bajeti ya Umoja huo, matumizi ya Umoja wa Ulaya yanatakiwa kupanda na suala la kilimo litatamalaki katika bajeti hiyo. Bajeti ya Ujerumani ikiwa na mtazamo wa kijamii ni mzigo kwa vijana. Nani , kama sio wao, watalipia malipo ya uzeeni ya ziada pamoja na mambo mengine yaliyomo. Chini ya uongozi wa kansela Angela Merkel sera za kijamii zinapata nguvu kuliko mishahara ya wafanyakazi.
Nalo gazeti la Märkische Oderzeitung la Frankfurt/Oder linazungumzia kuhusu miaka 200 ya kuzaliwa kwa Karl Marx. Mhariri anaandika:
"Hisia nzuri hususan kwa Wajerumani wenye umri mkubwa kutoka iliyokuwa Ujerumani mashariki kwa Marx haihusiani na kumbukumbu ya enzi ya DDR. Ni kuhusu hamu iliyopo baada ya kuwapo katika dunia bora zaidi, kuliko ahadi ya malipo. Usoshalisti , uhalisia wake , kwa wengi hauwezi kubadilishwa kama ulivyofikia mwisho wake. Kwa sababu mapinduzi katika nchi ambayo si sahihi , nchini Urusi, yalianzia, wakati mawazo hayo yalitumika vibaya ama wakati haukuwa sahihi.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman