Magazetini:Theresa May aahirisha mjadala wa Brexit Uingereza
11 Desemba 2018Tukianza na gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe , linazungumzia kuhusu mtafaruku unaojitokeza katika mchakato wa Brexit nchini Uingereza. Mhariri anaandika:
"Kuahirishwa ghafla kwa mjadala mkali kuhusiana na makubaliano ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya kumeepusha Theresa May kuagukia pua kisiasa na kudhalilika. Lakini fadhaa hiyo ya Brexit anairefusha tu. Waziri mkuu huyo wa Uingereza ana matumaini kwamba, kundi kubwa linaloongezeka la wakosoaji wake litakata tamaa. Wakati huo huo anataka kuongeza mbinyo kwa Umoja wa Ulaya, huku muda mfupi uliobakia hadi Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya Machi 29 kukisogea. Lengo la waziri mkuu ni kwamba, mataifa ya Umoja wa Ulaya yataipa Uingereza wakati ikijotoa vitu vitamu na kuzuwia kabisa Brexit ambayo ina masharti."
Waziri mkuu wa Uingereza ameweza kwa ukakamavu na bila kuyumbishwa kuendelea na mradi wake mkuu katika kipindi cha karibu miaka miwili na nusu ya utawala wake, anaandika hivyo mhariri wa gazeti la Schwäbische Zeitung la mjini Ravensburg. Mhariri anaendelea:
"Amefanya hivyo kutokana na matakwa ya wananchi ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na makubaliano na Umoja huo mjini Brussels. Makubaliano hayo ya kujitoa pamoja na ufafanuzi wa kisiasa ambao kwa washirika wengi wa Ulaya bara kwa kiasi kikubwa wanataka kupata maridhiano, wengine wakitaka kufika mbali zaidi katika muafaka. Mjini London lakini kuna hakuna kabisa hali ya muafaka na makubaliano. Wale wateteaji wakubwa wa Brexit ambao ni Boris Johnson na Jacob Rees-Mogg wanataka mwishoni mwa mwezi Machi kujitoa bila makubaliano yoyote. Hali hii inaweza kuleta matatizo makubwa ya kiuchumi kwa mataifa ya Ulaya pamoja na Ireland, na hata kwa Waingereza wenyewe."
Katika suala la mkataba wa Umoja wa Mataifa wa uhamiaji , mhariri wa gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung anaandika kwamba hofu kuhusu uhamiaji ni kuhusu utekelezaji. Mhariri anaandika:
"Kumekuwa na hali ya kupinga maelezo ya utekelezaji wa kutokulazimika kisheria, ambapo hatimaye unazungumzia tu kuhusu biashara ya bianadamu, kama ilivyo utaratibu hapa Ujerumani kwa muda mrefu. Mataifa mengi yako katika mbinyo kutokana na mkataba huu kuachana na siasa zao za kizalendo. Nchini Ubelgiji hali hiyo ilisababisha serikali kuporomoka. Ni hali ya uharibifu kimataifa. Iwapo tutaanza, kulazimika kuomba radhi, kwamba tuko katika hali mbaya ya dharura na kuonesha sura ya urafiki, mhariri anaandika kwamba, hapo hiyo si nchi yangu tena. Hayo ameyasema Angela Merkel mwishoni mwa mwaka 2015. Kuonesha urafiki kidogo, pia ni ubinadamu. Na hapo kuna mpaka. Na pia kuonesha ushirikiano wa pamoja kimataifa."
Mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung anazungumzia kuhusu mgomo wa madereva wa treni nchini Ujerumani. Mhariri anaandika:
"Matatizo mengi ya treni ni ya ndani. Lakini katika hali ya sasa ya mgomo wanaowajibika ni chama cha wafanyakazi wa huduma za treni. Wanapaswa kujiuliza , iwapo mgomo wao wa tahadhari wa nchi nzima ulikuwa ni sahihi. Hawakutilia maanani kuhusu wengi wa wasafiri kufika makazini na wakawasababishia matatizo makubwa. Mfumo mzima wa usafiri , iwe kwa reli, barabara, maji ama angani ulikuwa ulifikia ukomo wake. Hata hivyo ni mara chache kwa mfumo huo kufanyakazi bila matatizo."
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Josephat Charo