1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Mahakama Bangladesh yatoa waranti wa kumkamata Sheikh Hasina

17 Oktoba 2024

Mahakama moja ya Bangladesh imetoa waranti wa kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo aliye uhamishoni nchini India, Sheikh Hasina.

https://p.dw.com/p/4ltr8
Bangladesch Dhaka | Waziri Mkuu wa zamani Sheikh Hasina
Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh Sheikh HasinaPicha: Pavel Rahman/AP Photo/picture alliance

Kulingana na mwendesha mashtaka mkuu wa Bangladesh Mohammad Tajul Islam, waziri mkuu huyo wa zamani anastahili kukamatwa na kufikishwa mahakamani mnamo Novemba 18.

Hasina alikimbilia India baada ya kuondolewa madarakani na maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi.

Utawala wa miaka 15 wa Hasina ulishuhudia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kufungwa na kuuwawa kiholela kwa wapinzani wake wa kisiasa.

Hasina mwenye umri wa miaka 77 hajaonekana hadharani tangu alipoikimbia Bangladesh na mara ya mwisho alionekana katika kambi ya kijeshi karibu na mji mkuu wa India, New Delhi.