Mahakama Kenya yatulipilia mbali kesi dhidi ya mazao ya GMO
12 Oktoba 2023Oktoba mwaka 2022, serikali ya Kenya iliondoa marufuku ya muongo mmoja dhidi ya mazao ya GMO ili kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa uhakika wa chakula kufuatia ukame mbaya zaidi uliolikumba eneo la Pembe ya Afrika katika miaka 40.
Mwanasheria Paul Mwangi alifuangua kesi mahakamani, akisema uamuzi huo ni kinyume cha katiba kwasababu kulikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa mazao hayo.
Lakini hakimu wa mahakama ya mazingira Oscar Angote ameamua siku ya Alhamisi kuwa hakuna ushahidi wa kuonyesha madhara yoyote kwa mazingira au afya ya binadamu.
Kenya, kama mataifa mengine mengi ya Afrika, ilipiga marufuku mazao ya GMO kutokana na masuala ya afya na usalama na kulinda mashamba ya wakulima wadogo, ambayo ni sehemu ya wazalishaji wengi wa kilimo mashambani nchini humo.
Hata hivyo taifa hilo lilikabiliwa na ukosoaji kuhusiana na marufuku hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoka Marekani, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mazao ya GMO.