1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Mahakama Pakistan yabatilisha hukumu ya uhaini dhidi ya Khan

3 Juni 2024

Mahakama kuu ya Pakistan hii leo imebatilisha hukumu ya uhaini dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan, aliyeko gerezani kwa mashtaka mengine.

https://p.dw.com/p/4gb0d
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Mohsin Raza/REUTERS

Uamuzi huo wa majaji wawili katika Mahakama Kuu ya Islamabad ulitangazwa na Jaji Mkuu Aamer Farooq, hii ikiwa ni kulingana na mwandishi wa habari wa AFP aliyeshuhudia.

Wakili wa Khan, Salman Safdar amethibitisha uamuzi huo. Hata hivyo Khan anasalia gerezani akitumikia kifungo cha miaka 7 kwa kuvunja sheria ya Kiislamu kwa kumuoa Bushra Bibi muda mfupi baada ya kumtaliki mkewe mwingine.

Alikutwa pia na makosa ya ufisadi baada ya kupokea zawadi wakati akiwa Waziri Mkuu kati ya mwaka 2018 na 2022. Ingawa hukumu ya kifungo cha miaka 14 ilisitishwa mwezi Aprili, madai dhidi yake yangalipo.