1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Hong Kong yatoa hukumu kesi ya uchochezi

26 Septemba 2024

Mahakama ya Hong Kong imemhukumu mhariri mkuu wa Stand News Chung-Pui-kuen kifungo cha miezi 21 jela, huku kaimu mhariri mkuu wa zamani Patrick Lam akiachiliwa huru.

https://p.dw.com/p/4l7YY
Hong Kong I Chung Pui-kuen na Patrick Lam
Mhariri mkuu wa Stand News Chung-Pui-kuen na kaimu mhariri mkuu wa zamani Patrick Lam mjini Hong KongPicha: Vernon Yuen/NurPhoto/IMAGO

Lam ameachiwa baada ya hukumu yake kupunguzwa kwa sababu afya yake ni mbaya.

Mwezi uliopita waandishi hao wa habari walikuwa wa kwanza kutiwa hatiani chini ya sheria ya uchochezi ya enzi ya ukoloni tangu Hong Kong iliporejea kuwa chini ya utawala wa China mnamo 1997.

Watu 2 wakamatwa kwa uchochezi chini ya sheria ya usalama wa taifa Hong Kong

Chung na Lam walipatikana na hatia ya kula njama ya kuchapisha na kuchapisha tena machapisho ya uchochezi.

Walikabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela na faini ya dola 5,000 za Hong Kong, ambazo ni sawa na dola 640 za Marekani.