SiasaAfghanistan
Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa viongozi wa Taliban
23 Januari 2025Matangazo
Watuhumiwa ni pamoja na kiongozi wa juu wa kidini Haibatullah Akhundzada, ambao wanashutumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaaamu kufuatia hatua za kibaguzi dhidi ya wanawake na wasichana.
Ofisi ya mwendesha mashitaka Karim Khan imesema vidhibiti vilivyokusanywa kama sehemu ya uchunguzi vinatoa uthibitisho usio na shaka kwamba Akhundzada na Abdul Hakim Haqqani, aliyekuwa Jaji Mkuu tangu mwaka 2021 walihusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinaadamu na mateso kwa misingi ya jinsia.
Tangu kundi la kiislamu la Taliban nchini Afghanistan liliporejea madarakani 2021, limebana haki za wanawake, ikiwa ni pamoja na ukomo wa kusoma, kazi na uhuru wa jumla wa maisha ya kila siku.