1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya juu Kenya yaidhinisha ushindi wa Ruto

5 Septemba 2022

Mahakama ya juu nchini Kenya imetupilia mbali shauri la kisheria lililofunguliwa wiki iliyopita na mgombea aliyeshindwa wa muungano wa Azimio, Raila Odinga kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto.

https://p.dw.com/p/4GQfD
Kenia Wahlen 2022
Picha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Jaji Mkuu Martha Koome amesema Raila na walalamikaji wenzake wameshindwa kuithibitishia mahakama kwamba kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wa matokeo wakati wa mchakato wa uchaguzi.

Raila pamoja na walalamikaji wengine waliibua matakwa tisa wakihoji uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Uamuzi huo wa jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo unamfanya Ruto kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya na sasa anatarajiwa kuapishwa Jumanne ijayo.

Jaji Koome amesema mahakama hiyo itatoa maelezo ya kina kuhusu maamuzi hayo baada ya siku 21.