1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kenya yaagiza mch. Machenzie kubaki kizuizini

10 Mei 2023

Mahakama nchini Kenya imeamuru leo mhubiri Paul Nthenge Mackenzie anayetuhumiwa kwa vifo vya zaidi ya watu 130 awekwe kizuizini kwa wiki tatu zaidi.

https://p.dw.com/p/4RA3I
Kenya Kilifi | Wataalaamu na wapelelezi wakiwa wamebeba miili ya wanaohisiwa kuwa wafuasi wa kanisa la Good News International nchini Kenya.
Kisa cha kufukuliwa miili kidhaa katika msitu wa Shakahola kimewashtua wengi ndani na nje ya Kenya.Picha: Stringer/REUTERS

Mchungaji Paul Nthenge Mackenzie anakabiliwa na mashitaka ya ugaidi kuhusiana na kile kilichopewa kichwa cha "Mauaji ya Msitu wa Shakahola" baada ya ugunduzi wa kushtusha mwezi uliopita, wa makaburi ya pamoja karibu na mji wa Malindi. Mahakama ya Mombasa imeamuru Mackenzie, mkewe na washukiwa wengine 16 washikiliwe kwa siku 30. Hakimu Yusuf Shikanda alisema kuwaachia washukiwa hao kunaweza kuhujumu usalama wao pamoja na uchunguzi unaoendelea. Waendesha mashitaka walitaka awekwe kizuizini kwa siku nyingine 90. Jumla ya watu 133 mpaka sasa wamethibitishwa kufa, wengi wao watoto, baada ya wapelelezi kusema jana kuwa wamefukua miili mingine 21 kutoka kwenye eneo hilo la msitu.