SiasaNiger
Mahakama ya Niger yaondoka kinga ya kushtakiwa kwa Bazoum
15 Juni 2024Matangazo
Kulingana na rais wa mahakama hiyo, iliyoundwa mwezi Novemba na utawala mpya wa kijeshi, Abdou Dan Galadima, mahakama hiyo imeamuru kuondolewa kwa kinga ya Bazoum, aliyepinduliwa mwezi Julai 2023.
Mamlaka ya Niger inamtuhumu Bazoum kwa uhaini, kufadhili ugaidi na kupanga njama ya kuhujumu serikali. Amekuwa akizuiliwa kwenye makao ya rais kwenye mji mkuu Niamey tangu alipoondolewa madarkani Julai 26.
Kundi la mawakili wanaomwakilisha Bazoum limesema uamuzi huo unadhirisha ukiukwaji mkubwa wa haki nchini Niger.