1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Ufaransa yatoa waranti mpya wa kukamatwa kwa Bashar al-Assad

22 Januari 2025

Mahakimu wawili wa Ufaransa wametoa waranti wa kukamatwa dhidi ya kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Syria Bashar al-Assad kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/4pSUY
Bashar Al-Assad
Bashar al-AssadPicha: SANA/AP Photo/picture alliance

Chanzo kimoja kimesema hii ni hatua ya pili kama hiyo kuchukuliwa na mamlaka za haki za Ufaransa. Waranti huo wa kukamatwa umetolewa kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya mwalimu wa zamani raia wa Ufaransa aliyekuwa na uraia wa Syria na Ufaransa.

Salah Abou Nabout aliyekuwa na umri wa miaka 59, aliuwawa mnamo Juini 7 mwaka 2017 kufuatia kulipuliwa kwa nyumba yake na helikopta za jeshi la Syria.

Assad akimbia nchi, waasi waukamata Damascus

Kulingana na chanzo kimoja, ídara ya mahakama ya Ufaransa inachukulia kwamba Assad ndiye aliyeamrisha na kufadhili kufanyika kwa shambulizi hilo.

Maafisa wengine sita waandamizi katika jeshi la Syria tayari wametolewa waranti wa kukamatwa kuhusiana na kesi hiyo katika uchunguzi ulioanza mwaka 2018.