Mahama arejea Ikulu ya Accra
7 Januari 2025Matangazo
Kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 66, alishinda uchaguzi wa tarehe 7 Disemba kwa kiwango kikubwa cha kura, na hivyo kufanikiwa kurejea madarakani kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi linaloshikilia nafasi ya pili wa uzalishaji wa kakao.
Soma zaidi: Dramani Mahama ashinda uchaguzi Ghana
Mahama anachukuwa madaraka kutoka kwa Nana Akufo-Addo, ambaye anastaafu baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili, na hivyo kuendeleza utamaduni wa kidemokrasia wa Ghana, wa kubadilishana madaraka kwa njia za amani, katika eneo ambalo limetandwa na mapinduzi ya kijeshi na makundi ya uasi.
Kwa mara ya kwanza, Mahama aliingia madarakani mwaka 2012 kufuatia kifo cha Rais John Evans Atta-Mills, na kisha kushinda uchaguzi miezi michache baadaye.