Maharamia waichia meli Somalia
24 Mei 2024Taarifa hizo zilitolewa siku ya Ijumaa (Mei 24) na Shirika la Uendeshaji Biashara la Uingereza (UKMTO) bila ya kutaja jina la meli hiyo.
Hata hivyo, Kikosi cha Umoja wa Ulaya cha Kupambana na Ugaidi katika Bahari Hindi na Bahari ya Shamu kimesema watu wanaoshukiwa kuwa maharamia waliabiri meli ya kibiashara ya Basilisk yenye bendera ya Liberia katika eneo sawa na hilo siku ya Alhamisi (Mei 23).
Soma zaidi: Maharamia waiteka meli katika pwani ya Somalia
Umoja wa Ulaya ulisema kikosi chake kinachoendesha operesheni iitwayo Atlanta kilituma manuwari yake iliyokuwa karibu kukabiliana na tukio hilo.
Kati ya mwaka 2008 na 2018, maharamia wa Somalia walivuruga shughuli katika pwani ya taifa hilo.
Lakini kulikuwa kumeanza kupatikana utulivu hadi mwishoni mwa mwaka jana wakati matukio ya uharamia yaliripotiwa kuanza tena eneo hilo.