1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahojiano ya kansela na waandishi habari magazetini

Oumilkheir Hamidou
17 Julai 2017

Mahojiano kati ya kansela Merkel na waandishi habari, mwaka mmoja baada ya njama iliyoshindwa ya mapinduzi nchini Uturuki, na shambulio la wanamgambo wa itikadi kali dhidi ya watalii wa Ujerumani nchini Misri magazetini

https://p.dw.com/p/2geUx
Deutschland | ARD-Sommerinterview mit Angela Merkel
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Sohn

 

Tunaanzia na mahojiano aliyokuwa nayo kansela Angela Merkel na waandishi habari, mwishoni mwa wiki "mahojiano ya msimu wa kiangazi" kama yanavyoitwa.Yalikuwa mahojiano yanayotoa picha ya jinsi kansela alivyodhamiria kuendelea na mhula wake madarakani. Gazeti la Trierischer Volksfreund" linaandika: Anaemfuatilizia kwa makini kansela hatokosa kugundua jinsi alivyotulia,  jinsi anavyojiamini, akitambua fika wengi wa wajerumani wanataka nini. Ilani ya vyama ndugu vya Christian Democratic Union-CDU na Christian Social Union-CSU imetungwa kwa namna ambayo Merkel hatofuata njia nyengine isipokuwa ile wanayohisi ndiyo inayofaa. Analenga kuendeleza kile ambacho hadi wakati huu kimekuwa kikifanywa na serikali yake na kuwaridhisha wengi wa wananchi humu nchini.

Kampeni za uchaguzi mkuu zimepamba moto. Katika wakati ambapo kansela Angela Merkel anazungumza na waandishi wa habari, mgombea wa chama cha Social Democrat-SPD, Martin Schultz anajaribu kuipa msukumo kampeni ya chama chake inayosemekana imepwaya. Gazeti la "Landeszeitung" linaandika: "Martin Schulz amevuwa glovu za hariri na kuvaa zile za mbondia mnamo wiki kumi za mwisho za kampeni ya uchaguzi mkuu. Tatizo la mbinu hizo lakini ni kwamba suala la malumbano haliko mikononi mwake. Na ukweli huo umejitokeza katika mahojiano aliyokuwa nayo Angela Merkel. Hata kama hoja Schulz anazotoa ni muhimu, anapozungumzia kuhusu pengo katika usawa wa jamii, lakini wananchi wanaonyesha kuvutiwa zaidi na mada ya kuondoshewa pengo katika usalama. Na katika suala hilo la usalama wa ndani, SPD wanaonyesha bado ni dhaifu.

Udhaifu wa IS

Watalii wawili wa Ujerumani wamechomwa kisu na magaidi wanaojiita wa dola la kiislam nchini Misri. Gazeti la "Leipziger Volkszeitung" linalitaja shambulio hilo kuwa la "wenye woga". Ggazeti linaendelea kuandika: "Sasa ujumbe unageuza njia, unaelekezwa kwao wanaharakati wa IS: Hamna hata haya. Mtu mwenye kuwachoma kisu wanawake pwani, haonyeshi kama ana nguvu, anadhihirisha ni dhaifu. Hakuna udhaifu uliozidi huo. Sio lazma mtu awe na shahada ya uzamili katika faini ya saikolojia kuweza kugundua kwamba vituko kama hivyo havimaaminishi ujabari.

Mwaka mmoja baada ya njama ya mapinduzi iliyoshindwa

Uturuki imeadhimisha mwaka mmoja tangu ilipofanyika njama iliyoshindwa ya mapinduzi. Njama hiyo iliyoshindwa ya mapinduzi imeutia ila uhusiano kati ya Ujerumani na Uturuki. Gazeti la mjini Cologne linaandika: "Watu milioni nne wenye asili ya Uturuki wanaishi katika sahirikisho la jamhuri ya Ujerumani, wajerumani kadhaa wameoana na waturuki. Waturuki wanashiriki katika vyama vya kisiasa, vyama vya wafanyakazi na mashirika mengineyo ya jamii. Uhusiano huo utaendelea na hakuna yeyote atakaeweza kuuvunja.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu