Majadiliano ya upatanishi Kenya kuongozwa na Kofi Annan
20 Januari 2008NAIROBI: Hadi watu 2 wameuawa katika mapambano yaliyozuka kati ya makundi ya kikabila mjini Nairobi.Hayo ni sehemu ya machafuko yaliyotokea Kenya tangu Rais Mwai Kibaki kurejeshwa tena madarakani.Takriban watu 700 wameuawa tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanywa Desemba 27.Chama kikuu cha upinzani ODM kinasema,uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu.Mwenyekiti wa chama cha ODM amesema,chama hicho kimepanga kuwa na maandamano Alkhamisi ijayo kote nchini.
Wakati huo huo Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya,Louis Michel amekuwa na mikutano mbali mbali pamoja na Rais Kibaki na kiongozi wa ODM Raila Odinga.Baadae akasema,viongozi wote wawili wamekubali kushiriki katika majadiliano ya upatanishi yatakayoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan.