Majenerali Niger wamrejesha nyumbani balozi wake wa Abidjan
15 Agosti 2023Uamuzi huo umefikiwa kama hatua ya kuonesha upinzani kwa matamshi ya Ouattara ya kuunga mkono uamuzi wa Jumuiya ya ECOWAS wa kutuma kikosi cha kijeshi kuwalazimisha majenerali walioipindua serikali kuondoka madarakani.
Soma pia: Umoja wa Afrika unakutana kujadili mgogoro wa Niger
Kwenye matamshi hayo aliyoyatoa wiki iliyopita baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya ECOWAS, Ouattara pia alisema nchi yake itachangia kikosi cha askari 850 hadi 1,000 kuingilia kati kijeshi nchini Niger.
Katika hatua nyingine kundi moja la kutetea haki za binadamu nchini Niger limesema linashindwa kuwafikia maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya rais aliyepinduliwa Mohammed Bazoum ambao wanashikiliwa na utawala wa kijeshi. Kundi hilo limesema halifahamu hali za maafisa hao wanaojumuisha mawaziri na maombi yao ya kuwafikia hayajajibiwa.