Makanisa mazuri zaidi ya Ulaya
Makanisa ni chanzo cha mshangao, haswa wakati wa msimu wa Krismasi. Tanzama maeneo mazuri na maarufu ya ibada Ulaya.
Basilica ya Mtakatifu Petro huko Roma
Basilica ya Mtakatifu Petro iko katika Jiji la Vatican na ni moja ya makanisa saba ya hija mjini Roma. Uwanja wake ni takriban mita za mraba 20,000 na unaweza kuchukua watu wengi. Hii inafanya Basilica ya Mtakatifu Petro kuwa kubwa zaidi na pia inachukuliwa kuwa moja ya makanisa muhimu zaidi ulimwenguni.
Kanisa kuu la Milan
Duomo di Santa Maria Nascente ni moja ya majengo maarufu nchini Italia na moja ya makanisa makubwa zaidi ulimwenguni. Kipengele maalum ni paa, ambalo unaweza kufika kwa kulipa ada utalii. Ukiwa juu maandishi yaliyoandikwa kwenye mawe ya kanisa hilo unaweza kuyasoma vizuri sana. Pia inatoa mtazamo juu ya Milan nzima, hadi kwenye milima ya Alps ikiwa hakuna mawingu.
Kanisa kuu la Notre-Dame huko Paris
Ujenzi wa Notre-Dame de Paris ulichukua karibu karne mbili, kutoka 1163 hadi 1345, na kuifanya kuwa moja ya majengo ya zamani zaidi ya kanisa la Gothic huko Ufaransa. Kama sehemu ya ukingo wa mto wa Paris wa Seine, limekuwa Turathi ya Urithi wa Dunia wa UNESCO tangu 1991. Kanisa hilo lilipata uharibifu mkubwa baada ya kuungua mwezi Aprili 2019.
Sagrada Familia huko Barcelona
Pia inaitwa "haijakamilika" kwani ujenzi, ulioanza miaka 135 iliyopita, bado unaendelea. Hata hivyo, Sagrada Familia, iliyoundwa na Antoni Gaudí na Turathi ya Urithi wa Dunia wa UNESCO tangu 2005, huvutia mamilioni ya watalii kila mwaka. Usanifu wa asili wa Gaudí pengine hautakamilika kamwe.
Abbey ya Westminster huko London
Zaidi ya miaka 700, Westminster Abbey iko katikati mwa jiji la London. Ni hapo ambako wafalme na malkia wa Uingereza na Ireland ya Kaskazini wameapishwa, wamefunga ndoa na kuzikwa. Kutawazwa kwa mwisho hadi sasa ni kwa Malkia Elizabeth II mnamo Juni 2, 1953. Na mwaka 2011, Prince William na Kate walibadilishana viapo vya ndoa hapa.
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Cologne
Bila shaka, hakuna mtu anayetumia jina hili rasmi wakati unapotaja Kanisa Kuu la Cologne. Haikufuzu kabisa kwa jina la "kanisa refu zaidi nchini Ujerumani",kama Kanisa Kuu la Ulm, ambalo lina urefu wa mita 162.Lakini minara miwili ya mita 157 ni ya kuvutia hata hivyo. Kanisa kuu, lililojengwa kutoka 1248 hadi 1880,halionekani mara kwa mara bila kiunzi kwani kila wakati kuna kitu kinachorekebishwa.
Kanisa la Mama Yetu huko Dresden
Frauenkirche (Kanisa la Mama Yetu), lilijengwa kutoka 1726 hadi 1743 na linachukuliwa kuwa jengo kuu la mtindo wa Baroque wa Dresden. Mwishoni mwa Vita vya pili vya dunia, liliharibiwa vibaya na mashambulizi ya anga. Liliungua na kuporomoka Februari 15,1945. Baada ya Mapinduzi ya Amani katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, lilijengwa upya kuanzia 1994.
Kanisa kuu la Mtakatifu Stephen huko Vienna
Ujenzi wa alama hii ya Viennese ulianza katika karne ya 12 na ulidumu kwa karne kadhaa. Leo, Kanisa Kuu la Mtakatifu Stephen linachukuliwa kuwa mojawapo ya majengo mashuhuri zaidi ya Kigothi huko Austria.Hatua 343 zinaongoza hadi kwenye chumba cha turret, ambapo kuna mtazamo wa kuvutia juu ya Vienna. Kengele ya pili kwa ukubwa barani Ulaya inaning'inia kwenye mnara.
Kanisa kuu la St. Vitus huko Prague
Kanisa Kuu la Mtakatifu Vitus huko Prague, kanisa kubwa na maarufu zaidi katika Jamhuri ya Czech, liko katika uwanja wa Kasri wa Prague. Mashujaa kadhaa wa kitaifa, wafalme na watakatifu wamezikwa kwenye kanisa kuu. Miongoni mwao St. Nepomuk. Kanisa Kuu la St. Vitus pia linahifadhi moja ya hazina muhimu zaidi za kanisa kuu la Ulaya.
Kanisa la Ufufuo huko St Petersburg
Kanisa la Ufufuo ndilo jengo kuu pekee la kanisa katikati mwa jiji la St.Petersburg. Lilijengwa kutoka 1883 hadi 1912 kwenye taruthi ambayo Tsar Alexander II aliuawa mnamo 1881.
Kanisa la Borgund Stave huko Norway
Katika jimbo la Norway la Vestland linasimama moja ya majengo ya zamani zaidi ya mbao huko Ulaya. Kanisa la Borgund Stave ni mojawapo ya mifano bora zaidi ya usanifu wa Stave huko Norway. Kanisa liko wazi kwa wageni kutoka Mei hadi Septemba. Kando yake kuna kituo cha habari kuhusu historia ya makanisa ya stave na dini katika Enzi za Kati.