Wapatanishi wa mazungumzo ya kuufufua mkataba wa amani wa Sudan Kusini wa mwaka 2015, wamesema mazungumzo hayo yamemalizika Jumatano bila ya kufikiwa makubaliano. Wapatanishi hao kutoka IGAD, wamesema hali hiyo inaweza kuchangia kuendelea kwa vita. Je hali hiyo inaiweka wapi Sudan Kusini? Sikiliza mahojiano haya kati ya Grace Kabogo na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Kenya Martin Oloo.